Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Josphine Manase amewataka wauguzi wote Wilayani Kyela kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uzalendo, huku akisisitiza umuhimu wa kulinda miiko na maadili ya taaluma ya uuguzi ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza leo Mei 17, 2025 katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika Kiwilaya Katika Hospitali ya Matema, Mhe. Manase amewaasa wauguzi kuendelea kuwa na nidhamu ya kazi, kuheshimu wateja wao, na kuhakikisha wanatoa huduma kwa huruma, upendo na ufanisi bila kujali changamoto zilizopo katika mazingira yao ya kazi.
Mhe.Manase Amefafanua kuwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mama mchapakazi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya ikiwemo ununuzi wa Vifaa tiba vya Kisasa na Majengo Bora hivyo bila ya kuwepo kwa huduma nzuri na bora kutoka kwa watoa huduma za afya, na hasa Wauguzi, uwekezaji huu hautakua na tija kwa Wananchi.
Hatahivyo Mhe. Manase amewaasa Wauguzi Wilayani Kyela kutumia Mfumo wa Pepmis kujaza taarifa zao zinazotakiwa ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa pindi unapofika muda wakupanda Madaraja kazini.
Vilevile Mkuu wa Wilaya amewataka Wauguzi hao kuendelea kutoa Elimu bila kuchoka Kwa jamii dhidi ya Mila potofu hasa kwa wakina Mama wajawazito waache kutumia Mitishamba wanayoiamini kuwa inawarahisishia kujifungua kwa urasi bila kufika katika Vituo vya kutolea huduma za afya badala yake watumiaji wa dawa hizo za kienyeji hupata matazo makubwa wakati wa kujifungua.
Aidha, Wauguzi hao walitumia fursa hiyo kuhuisha Uuguzi wao kwa kula kiapo upya na kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kuendelea kumuenzi muasisi wa kada ya Uuguzi Bi. Florence Nightingale
Sanjari na hayo Wauguzi hao walipata wasaa wa kuwasilisha Zawadi yao kwa Mkuu wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Kyela Ndg. Saumu Seif Kumbisaga ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kujali na kuwathamini watoa huduma za Afya Wilayani Kyela
Ikumbukwe kuwa Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani hufanyika kila mwaka Mei 12 ili kutambua mchango mkubwa wa wauguzi katika sekta ya afya duniani kote.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa