Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe.Josephine Manase amefungua mafunzo elekezi kwa Wajumbe wa baraza la Mamlaka ya mji mdogo wa Kyela katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka tarehe 14.2.2025
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mhe.Mkuu wa Wilaya amewapongeza Wajumbe kushiriki na kupata nafasi kuwa wajumbe,pia amewataka Wajumbe hao kufuata kanuni na Sheria za uongozi ili waweze kuongoza vyema kwenye maeneo yao.
Mhe.Mkuu wa Wilaya amewaagiza Wajumbe kujenga ushirikiano mzuri na Wananchi katika utendaji kazi ili kujua na kutatua changamoto zinazowakabili.
Aidha Mhe.Mkuu wa Wilaya amewataka wajumbe hao kuweka utaratibu wa kufanya vikao vya mara kwa mara na wananchi kwani vikao hivyo ni chachu ya maendeleo endelevu kwa vitongoji na Wilaya kwa ujumla.
Sambamba na hilo Mhe.Josephine Manase amewataka wajumbe wa Mamlaka kuwa wasemaji wazuri kwa Wananchi juu ya miradi ya maendeleo inayojengwa kupitia fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,ili wananchi waweze kutunza miradi hiyo.
Kuhusu ukusanyaji wa mapato Mhe.Mkuu wa Wilaya amewataka wajumbe hao kuwa wasimamizi wazuri wa mapato ili kujenga maslahi ya mamlaka kwa ajili ya kujenga uchumi na maendeleo ya Mamlaka na Wilaya.
Akisisitiza suala la lishe Shuleni Mhe. Josephine Manase amewataka Wajumbe kutoa elimu kwa Wazazi wenye watoto shuleni kutoa mchango wa chakula ili watoto waweze kupata chakula wawapo shuleni ikiwa ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya suala la kuondoa udumavu.
Akifunga mafunzo ya Wajumbe wa Mamlaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Florah A.Luhala amewataka wajumbe kuwa mfano bora na kusimamia vyema masuala muhimu kwenye maeneo yao ikiwemo kutoa elimu kwa Wananchi juu ya ukusanyaji mapato,na umuhimu wa usafi wa mazingira.
Pia Mkurugenzi Mtendaji amewataka wajumbe kufuata kanuni na sheria kama walivyoelekezwa na wawezeshaji wa mafunzo hayo.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa