Wilaya ya Kyela imeadhimisha siku ya UKIMWI duniani tarehe 30/11/2023 katika kata ya Mababu kijiji cha Ngyeke.
Akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Mkuu wa wilaya ya Kyela, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mhe. Katule G. Kingamkono, amewapongeza viongozi wa wilaya na wananchi kwa jitihada za utoaji wa elimu ya kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya VVU, hatimae wilaya ya Kyela imeshuka katika takwimu za maambukizi mapya kutoka 3.4% mwaka 2021/2022 hadi kufikia 2.7% kwa mwaka 2022/2023.
Aidha amewataka akinamama wajazito kuwahi kufika vituo vya afya ili kupima afya zao afya na pindi wanapogundulika kuwa na maambukizi ni vyema wakaanza kutumia dawa ili kumkinga mtoto.
Pia amewashauri wananchi kuendelea kutokupima UKIMWI tu bali, wapime hata magonjwa mengine pamoja na kuzingatia suala la tohara ili kulinda Afya.
Vilevile Mheshimiwa Katule amewasisitiza wananchi kufanya mazoezi na kuzingatia mlo kamili kwa faida ya kuimarisha afya ya mwili.
Awali Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe (W) Dr. Proneth Mtei amesema;
Wilaya ya Kyela imeendele kupambana na janga la UKIMWI, kwa kutekeleza afua mbalimbali za kudhibiti maambukizi mapya ikiwemo kutoa elimu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa jamii.
Kutoa dawa kinga kwa makundi maalumu, kutoa huduma ya tohara ya hiari kwa wanaume wenye umri miaka 15 nakuendelea kwani hupunguza maambukizi kwa 60%, Ugawaji na usambazaji wa kondom.
Aidha amesema kutokana na hayo kuna manufaa yamepatikana ikiwemo wananchi kujua hali zao za afya, kupunguza vifo vitokanavyo na VVU/UKIMWI pia kuwepo na jamii yenye afya na kujiletea maendeleo.
Mwisho.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa