Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa (Katikati) akiangalia moja ya kitalu cha miche ya Kakao kilichopo kata ya Ipinda wilayani Kyela.
Wilaya ya Kyela imetekeleza agizo la Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, agizo lililotolewa tarehe 03/08/2021, ambalo lilimtaka Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya kuhakikisha anazalisha miche ya kakao na kuigawa bure kwa wakulima wilayani hapa.
Akikabidhi miche hiyo kwa baadhi ya wakulima, Mkuu wa wilaya ya Kyela Mheshimiwa Ismail Mlawa mesema, amegawa miche ya kakao kwa wakulima huku akiamini miche hiyo imetokana na mbegu bora, "ukiwa na uchumi mzuri katika wilaya unakuwa na uhakika wakuwa na wananchi wenye maisha bora, Pia wanakuwa na uwezo wa kuwapeleka watoto wao shule, kupata chakula cha uhakika na kupata huduma za afya bora" alisema.
Aidha alisema hakuna sababu wanaKyela kukaa vijiweni kwa sababu Kyela imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba, hivyo wananchi hatutakiwi kubweteka yatupasa kufanya kazi.
Pia aliwaomba chama kikuu cha ushirika Kyela (KYEKU), kuongeza jitihada za kuzalisha miche ya kakao ili kila mkulima aweze kupata miche hii mipya na kuachana na ile ya zamani iliyozeeka.
Nae mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono amewaambia wakulima kwamba, kwa kupitia Baraza la Waheshimiwa Madiwani, wamejipanga kwa kupitia mapato ya ndani, kuanza kuwekeza nguvu katika kilimo hususani katika uzalishaji wa miche ya kakao na michikichi, hivyo wakulima wakae mkao wa kula.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Mheshimiwa Katule G. Kingamkono akiongea na baadhi ya wakulima kabla ya zoezi la kuwakabidhi miche ya kakao katika kata ya Ipinda Kyela.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima ndugu Jackson Gelevasi amesema wakulima wanawaomba watalaam wa kilimo kuwapitia wakulima katika mashamba yao ili kuweza kuwapa ushauri kwa ajiri ya Kuboresha zao hilo.
Chama Cha Ushirika Kyela (KYEKU) kimezalisha miche 13,510 ya kakao ikiwa ni miche 3510 zaidi kwa ajiri ya kufisia miche iliyokufa na kuharibika.
Moja ya kitalu safi cha miche ya kakao kilichopo kata ya Ipinda Kyela, ambacho miche yake itagawiwa kwa wakulima.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa