Mkuu wa wilaya ya Kyela Me. Claudia U. Kitta, amepokea madawati zaidi ya 150, yaliyotolewa na Benki ya NMB hapa wilayani Kyela tarehe 10/10/2019.
Madawati hayo yamegawiwa katika shule 3, za sekondari yaani shule ya srkondari Ikimba, iliyopo kata ya Njisi wilayani hapa, shule ya sekondari Masukila iliyopo kata ya Ngana pamoja na shule ya sekondari Nkuyu, iliyopo katika kata ya Nkuyu wilayani hapa. Wakati huo huo Benki ya NMB, imetoa mabati zaidi ya 160 katika shule ya sekondari Itunge iliyopo kata ya Itunge wilayani hapa.
Akipokea madawati hayo, Mkuu wa wilaya ya Kyela amewataka wanafunzi, kuyatunza madawati hayo kwani, wanafunzi wengi wamekuwa ni waharibifu wa miundo mbinu ya shule.
Pia amewataka wanafunzi kujijengea ukuta mzuri wa kujitunza katika vichwa vyao na sio, kusubili kusukumwa kwa kila kitu, hivyo aliwasisitiza kujitambua.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa