Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela ndugu Ezekiel Magehema (katika)akipokea maelekezo kutoka kwa engineer wa ujenzi wa wodi la wazazi katika hospital ya wilaya ya Kyela.
Wakuu wa Idara na vitengo wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela, wamepata fulsa ya kufanya ziara katika katika jengo la wodi ya akina mama linalojejengwa la katika hospital ya wilaya ya Kyela, ziara hii imefanyika tarehe 13 /10/2020.
Akiongea na watumishi wenzake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kyela ndugu Ezekiel Magehema amesema,
Ameamua kufanya ziara akiwa na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali vya halmashauri, ili kufanya uongozi shirikishi ambao utamfanya kila mkuu wa Idara au kitengo kujua na kuelezea hatua mbalimbali zinazoendelea katika ujenzi huo. Pia amebainisha kwamba hadi kufikia hatua iliyopo sasa, jengo hili limeshatumia zaidi ya shilingi milioni 400,000,000/=Tshs na ujenzi upo hatua ya msingi.
Aidha ameongeza kwa kusema ni vizuri kila mfanyakazi au mkuu wa Idara na vitengo kufahamu ujenzi unavyofanyika kwa kila hatua, kwani kuna baadhi ya hatua za ujenzi hazita onekana kama zimefanyika baada kuanza kwa ujenzi wa hatua mpya.
Hivyo ni vema tukashirikiana kufahamu haya, ili utowaji wa Maelezo juu ya ujenzi huu ukafanana kwa watumishi wote.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa