Shirika la Starkey Hearing Foundation la Marekani kwa kushirikiana na chama cha Tanzania Society for the Deaf(TSD) wametoa huduma ya afya kwa kuwachunguza wanafunzi 8 kati ya 30, ambao ni viziwi. Huduma hii ilitolewa Mjini Dar es salaam, ambapo wanafunzi hao walipelekwa na Afisa elimu elimu maalum Kyela (DSNEO) ndugu Kanzale L. Mwangungulu.
Aidha mwalimu huyo amesema, wanafunzi hao waliweza kupewa msaada wa vifaa vitakvyowasaidia wanafunzi kuweza kusikia yaani (Hearing Aids) vyenye gaharama ya shilingi milioni 5,550,000/=.
Hata hivyo mahitaji ya vifaa hivyo bado ni makubwa sana kwani kati ya wanafunzi 30, walioweza kupewa vifaa hivyo ni wanafunzi 8 tu, ambao ni Daniel Mwakobela, Romanus Nkwela kutoka shule ya msingi Kyela, Maza Mwamwenda, Debora Lwitiko, Grory Namkese, Anton Mwakisambwe, Fredy Mwakalenge wote wa shule ya msingi Mwenge iliyopo kata ya Ipinda Kyela, pamoja na Aizack Mwambeje wa shule ya msingi Ikolo.
Afisa elimu msingi wa wilaya ya Kyela (kushoto) ndugu Palemon Ndarugiliye akiwa na moja ya mwanafunzi mnufaika ofisini kwake.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa