Kutokana na mvua zinaendelea kunyesha katika wilaya ya Kyela zikiungana na zile zinazonyesha wilayani Rungwe, ambazo hapa Kyela zilianza tarehe 10/05/2019 mpaka leo, mvua hizi zimesababisha usumbufu mkubwa wilayani hapa.
Kata zaidi ya tano zimekumbwa na mafurikao haya, zikiwemo kata ya Bujonde, Kajujunjumele, Katumbasongwe, Talatala na Ikama.
Nyumba nyingi zimeingiliwa na maji, vyombo vimesombwa na maji pamoja na baadhi ya mashamba kuharibiwa kwa kuwango cha kutisha.
Aidha kamati ya maafa ya wilaya ya Kyela ikiongozwa na Mkuu wa wilaya Mhe. Claudia U. Kitta, ameongozana na viongozi wengine na kufanya ziara katika maeneo yote yaliyoathirika, ili kutoa pole na kufanya tathmini ya kutoa misaada kwa waathirika wote.
Hadi kufikia tarehe 12/05/2019 jumla ya kaya 438 zenye wakazi zaidi ya 2570, zilihamishwa na kuwekwa mahali salama, kwa mfano katika makambi, ofisi mbalimbali za serikali na katika baadhi ya shule.
Hata hivyo wilaya ya Kyela kupitia viongozi wake wameanza kutoa misaada ya chakula na dawa za maji ili kulinda afya za Wananchi walioathirika na mafuriko hayo.
Imetolewa na :
Ofisi ya Habari na Mawasiliano
Kyela.
Bomani Street
Sanduku la Posta: P. O box 320 Kyela
Simu ya Mezani: 025-2540035/7
Simu ya Mkononi: 0713655466
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Kyela. Haki zote zimehifadhiwa